Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 8:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Malaika wa nne akapiga baragumu, thuluth ya jua ikapigwa, na thuluth ya mwezi, na thuluth ya nyota, illi ile thuluth itiwe giza, mchana usiangaze thuluth yake wala usiku vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kisha, malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng'ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga, hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kisha, malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng'ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga, hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kisha malaika wa nne akaipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua, theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota zikapigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga ikawa giza. Theluthi ya mchana ikawa haina mwanga na pia theluthi ya usiku.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 8:12
26 Marejeleo ya Msalaba  

Marra baada ya shidda ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbingu zitatikisika:

Tangu saa sita palikuwa giza juu ya inchi yote hatta saa tissa.

Lakini siku hizo baada ya shidda ile jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake,

Ilipokuwa saa sita, pakawa na giza juu ya inchi yote, hatta saa tissa.

Na kutakuwa ishara katika jua na mwezi na nyota: na katika inchi dhiiki ya mataifa, wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;

Jua litageuka kuwa giza, Na mwezi kuwa damu, Kabla ya kuja ile siku ya Bwana Iliyo kuu, dhahiri.

ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

Na mkia wake wakokota thuluth ya nyota za mbinguni na kuziangusha katika inchi.

Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao,

Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,

Wale malaika wane wakafunguliwa, waliowekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka illi waue thuluth ya wana Adamu.

Thuluth ya wana Adamu wakauawa kwa matatu bayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho kilichotoka katika vinywa vyao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo