Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 7:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kisha, nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: Watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kisha, nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: Watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kisha, nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuwahesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 7:9
41 Marejeleo ya Msalaba  

HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


wakatwaa matawi ya mitende wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana; Amebarikiwa ajiie kwa jina la Bwana, mfalme wa Israeli.


Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili;


Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kutimiza yote kusimama.


Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, nae kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufukoni, usioweza kuhesabiwa.


Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


Wala hapatakuwa laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana kondoo kitakuwa ndani yake.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale nyama wenye uhayi, na za wale wazee, na hesabu yao, elfu kumi marra elfu kumi, na elfu marra elfu,


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Wa kabila ya Zabulon thenashara elfu. Wa kabila ya Yusuf thenashara elfu. Wa kabila ya Benyamin thenashara elfu waliotiwa muhuri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo