Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 7:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uhai. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uhai. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uhai. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa maana Mwana-Kondoo aliyeko katikati ya kile kiti cha enzi atakuwa Mchungaji wao; naye atawaongoza kwenda kwenye chemchemi za maji yaliyo hai. Naye Mungu atawafuta machozi kutoka machoni mwao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa maana Mwana-Kondoo aliyeko katikati ya kile kiti cha enzi atakuwa Mchungaji wao; naye atawaongoza kwenda kwenye chemchemi za maji yaliyo hai. Naye Mungu atafuta kila chozi kutoka macho yao.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 7:17
42 Marejeleo ya Msalaba  

Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli.


Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika.


Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema: mchunga aliye mwema huweka maisha yake kwa ajili ya kondoo.


Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema; na walio wangu nawajua, na walio wangu wananijua,


Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi?


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


lichungeni kundi la Kristo lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa khiari; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo;


Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo.


Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyiezi ni hekalu lake, na Mwana kondoo.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo.


Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Umestahili, Bwana, Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na nweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, vikaumbwa.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo