Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 7:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BAADA ya haya nikaona malaika wane wamesimama katika pembe nne za inchi, wakizizuia pepo nne za inchi, upepo usivume juu ya inchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za dunia, wakishika pepo nne za dunia ili upepo usivume hata kidogo: Wala katika nchi, wala baharini, wala kwenye miti.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za dunia, wakishika pepo nne za dunia ili upepo usivume hata kidogo: Wala katika nchi, wala baharini, wala kwenye miti.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za dunia, wakishika pepo nne za dunia ili upepo usivume hata kidogo: wala katika nchi, wala baharini, wala kwenye miti.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wowote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wowote.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 7:1
23 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.


Ndipo atakapowatuma malaika zake na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa inchi hatta upande wa mwisho wa mbingu.


nae atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za inchi, Gog na Magog, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.


Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo.


akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.


Malaika wa kwanza akapiga baragumu, kukawa mvua ya mawe na moto vilivyotangamana na damu, vikatupwa juu ya inchi: thuluth ya miti ikateketea, majani mabichi yote yakateketea.


ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue malaika wane waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrati.


Wakaambiwa wasiyadhuru majani ya inchi wala kitu cho chote kilicho kibichi, wala mti wo wote, illa wale watu wasio ua muhuri ya Mungu katika vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo