Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 6:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Akatoka farasi mwingine mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katikii inchi, watu wauawe, akapewa upanga mkubwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpandafarasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpandafarasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nami nikatazama na kumbe palikuwapo farasi mwingine hapo, mwekundu. Mpandafarasi wake alikabidhiwa jukumu la kuondoa amani duniani, watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ndipo akatokea farasi mwingine mwekundu sana. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ndipo akatokea farasi mwingine mwekundu sana. Yeye aliyempanda akapewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye akapewa upanga mkubwa.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 6:4
17 Marejeleo ya Msalaba  

Msidhani ya kuwa nalikuja kueneza amani duniani; la! sikuja kueneza amani, bali upanga.

Na mtasikia khabari za vita na uvumi wa vita: angalieni, msitishwe: maana haya hayana buddi kuwa; lakini mwisho wenyewe hado.

Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.

Ishara nyingine ikaonekana mbinguni; joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba.

Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu.

Akanichukua katika Roho hatta jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu va nyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya ukafiri, mwefiye vichwa saba na pembe kumi.

Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo