Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 6:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana upinde, akapewa taji, akatoka, akishinda na apate kushinda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpandafarasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi, aendelee kushinda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpandafarasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi, aendelee kushinda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mimi nikatazama, na kumbe palikuwa na farasi mmoja mweupe hapo. Na mpandafarasi wake alikuwa na upinde, akapewa na taji. Basi, akatoka kama mshindi, aendelee kushinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nikatazama, na hapo mbele yangu palikuwa na farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upinde, naye akapewa taji, akampanda akatoka akiwa kama mshindi aelekeaye katika kushinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Nikatazama, na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mweupe! Yeye aliyempanda alikuwa na upinde, naye akapewa taji, akampanda akatoka akiwa kama mshindi aelekeaye katika kushinda.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 6:2
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia.


Maana sharti amiliki yeye, hatta awaweke maadui wote chini ya miguu yake.


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.


Nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwana Adamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali.


Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Na majeslii yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa katani safi, nyeupe.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Na maumbo ya zile nzige kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama taji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao kama nyuso za wana Adamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo