Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 6:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watauawa kama wao wenyewe walivyouawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watauawa kama wao wenyewe walivyouawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Wakapewa kila mmoja vazi refu jeupe, wakaambiwa wazidi kusubiri kwa muda mfupi, mpaka itakapotimia idadi ya watumishi wenzao na ndugu ambao watauawa kama wao wenyewe walivyouawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe na wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, hadi idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe na wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouawa kama wao walivyouawa, itakapotimia.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 6:11
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na ndugu atamsaliti ndugu apate kufa, na baba atamsaliti mtolo; na watoto wataondoka kuwashitaki wazee wao, wawafishe.


Lakini baba yake akawaambia watumishi wake, Ileteni joho iliyo bora, mkamvike: mpeni pete kwa kidole chake na viatu kwa miguu yake.


Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada.


Lakini siyahesabu maisha yaugu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na khuduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


Nimevifanya vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;


kwa kuwa Mungu ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, illi wasikamilishwe pasipo sisi.


na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,


Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarche mwenyewe baada ya kazi yake, kama vile Mungu alivyostarche baada ya kazi zake.


akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya,


Akapewa kutia pumzi katika sanamu ya nyama, hatta ile sanamu ya nyama inene, na kufanya wo wote wasioisujudu sanamu ya nyama wanawe.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.


Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo