Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 6:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kisha, nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe hai wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kisha, nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe hai wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kisha, nikamwona Mwanakondoo anavunja mhuri mmojawapo wa ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe hai wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo, “Njoo!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Nikaangalia Mwana-Kondoo alipofungua ule muhuri wa kwanza miongoni mwa mihuri saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha nikaangalia wakati Mwana-Kondoo akivunja ile lakiri ya kwanza miongoni mwa zile saba. Ndipo nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akisema kwa sauti kama ya radi: “Njoo!”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 6:1
17 Marejeleo ya Msalaba  

Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni kama santi ya maji mengi na kama sauti ya radi kuu. Nikasikia sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao:


Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Halleluya; kwa kuwa Bwana Mungu Mwenyiezi amemiliki.


Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.


NIKAONA katika mkono wa kuume wa aliyeketi juu ya kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.


wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.


Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.


Na alipofungua muhuri ya pili, nikamsikia nyama wa pili akisema, Njoo uone.


Na alipoifungua muhuri ya tatu nikamsikia nyama wa tatu mwenye uhayi akisema, Njoo, none. Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.


Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya nyama wa nne akisema, Njoo uone.


HATTA alipofungua muhuri ya saba kukawa kimya mbinguni kama muda wa nussu ya saa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo