Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 5:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Kisha nikaona pale katikati ya kiti cha enzi Mwanakondoo amesimama, akizungukwa kila upande na wale viumbe hai wanne, na wale wazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba ambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwa kila mahali duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Kisha nikaona pale katikati ya kiti cha enzi Mwanakondoo amesimama, akizungukwa kila upande na wale viumbe hai wanne, na wale wazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba ambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwa kila mahali duniani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Kisha nikaona pale katikati ya kiti cha enzi Mwanakondoo amesimama, akizungukwa kila upande na wale viumbe hai wanne, na wale wazee. Huyo Mwanakondoo alionekana kana kwamba amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba ambayo ni roho saba za Mungu zilizokuwa zimepelekwa kila mahali duniani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba za Mungu zilizotumwa duniani pote.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 5:6
35 Marejeleo ya Msalaba  

Ametuondokeshea wokofu wa nguvu Katika nyumba ya Daud mtumishi wake.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Akamtazama Yesu, akitembea, akasema, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu!


Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili: Alichukuliwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana kondoo asivyolia mbele yake amkatae manyoya, Vivyo hivyo yeve nae hafunui kinywa chake.


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyiezi ni hekalu lake, na Mwana kondoo.


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Wala hapatakuwa laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana kondoo kitakuwa ndani yake.


Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.


Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale nyama wenye uhayi, na za wale wazee, na hesabu yao, elfu kumi marra elfu kumi, na elfu marra elfu,


wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.


Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele.


Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.


wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo