Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 5:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na mmoja wa wale wazee akaniambia, Usilie, tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, shina la Daud, yeye amepata uwezo wa kukifunua kitabu na kuzivunja zile muhuri saba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, chipukizi wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, chipukizi wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kisha mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama! Simba wa kabila la Yuda, chipukizi wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kuivunja mihuri yake saba na kukifungua hicho kitabu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja mihuri yake saba.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 5:5
25 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akawageukia, akasema, Binti za Yerusalemi, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.


Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.


Akasema, Msilie; kwa maana hakufa, bali amelala usingizi.


Nao wakamwambia, Bibi, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala sijui walikomweka.


khabari za Mwana wake, aliyekuwa katika ukoo wa Daud kwa jinsi ya mwili,


Na tena Isaya anena, Litakuwa shina la Yesse, Nae aondokeae kuwatawala Mataifa; ndiye Mataifa watakaemtumaini.


Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote la kuikhusu katika mambo ya ukuhani.


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifuugua kitabu na kukisoma, wala kukitazama.


NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone.


Akajibu mmoja wa wale wazee akaniambia, Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni nani? na walikotoka wapi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo