Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 5:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini – viumbe vyote ulimwenguni – vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi, milele na milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini – viumbe vyote ulimwenguni – vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi, milele na milele.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini — viumbe vyote ulimwenguni — vikisema: “Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo, iwe sifa na heshima na utukufu na enzi, milele na milele.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi, na baharini, na vyote vilivyomo, vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aliyeketi juu ya hicho kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 5:13
29 Marejeleo ya Msalaba  

Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amin.


yeye ndiye Mungu mwenye hekima peke yake; na atukuzwe kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amin.


na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.


kwake yeye utukufu katika Kanisa, na katika Kristo Yesu hatta vizazi vyote vya milele na milele. Amin.


illi kwa jina la Yesu killa goti likunjwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya inchi;


mkidumu tu katika imani, mmewekwa juu ya misingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia khabari zake, iliyokhubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paolo nalikuwa mkhudumu wake.


Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.


Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.


Uweza una yeye hatta milele na milele. Amin.


Yeye aliye Mungu pekee, mwenye hekima, Mwokozi wetu: kwake yeye utukufu, na ukuu, na uwezo, na nguvu kwa Yesu Kristo, tangu milele, na sasa, na hatta milele. Amin.


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


NIKAONA katika mkono wa kuume wa aliyeketi juu ya kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.


wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.


Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya inchi, wala chini ya inchi, aliyeweza kukifunua kitabu wala kukitazama.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo