Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 4:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja, na walikuwa wamejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika, huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja, na walikuwa wamejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika, huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Viumbe hao wanne walikuwa na mabawa sita kila mmoja, na walikuwa wamejaa macho, ndani na nje. Usiku na mchana, bila kupumzika, huimba: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako, aliyeko na anayekuja!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko, na atakayekuja.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kila mmoja wa hawa viumbe wanne wenye uhai alikuwa na mabawa sita, na kujawa na macho pande zote hadi chini ya mabawa. Usiku na mchana hawaachi kusema: “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni bwana Mwenyezi Mungu, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 4:8
42 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi.


Nami nitawakaribisheni, Nitakuwa Baba kwenu, Na ninyi mtakuwa kwangu wana na binti, anena Bwana Mwenyiezi.


Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu.


Jitunze nafsi yako, na yale mafundisho. Ukadumu katika hayo; maana kwa kufanya hivi utajiokoa nafsi yako nao wakusikiao.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Yesu Kristo, jana na leo yeye yule na hatta milele.


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


wakisema, Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyiezi, ulioko, na nliyekuwako, kwa sababu umetwaa uweza wako ulio mkuu, ukamiliki.


Na moshi wa maumivu yao wapanda juu hatta milele na milele, nao bawana raha mchana na usiku, bao wamsujuduo nyama na sanamu yake, na killa aipokeae alama ya jina lake.


nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi.


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele.


Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi.


Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


Na wale wazee ishirini na wane, na wale nyama wane wenye uhayi wakasujudu na kumwabudu Mungu aketiye katika kiti cha enzi, wakisema, Amin, Halleluya.


Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyiezi ni hekalu lake, na Mwana kondoo.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma.


Na hawa nyama wenye uhayi watakapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi yeye aliye hayi hatta milele na milele ntukufu na heshima na shukrani,


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone.


Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo.


Na malaika wote wamesimama pande zote za kiti cha enzi na za wazee na za vile viumbe vine vyenye uhayi, wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,


Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda khema yake juu yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo