Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 4:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Na mliele ya kile kiti cha enzi, mfano wa bahari ya kioo eheupe, kama krustallo, na kati kati ya kile kiti cha enzi, na pande zote za kile kiti, nyama wane, wamejaa macho mbele na nyuma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe ling'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kulikuwa na viumbe hai wanne. Viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe ling'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kulikuwa na viumbe hai wanne. Viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na kitu kama bahari ya kioo, angavu kama jiwe ling'aalo sana. Katika pande zote za hicho kiti cha enzi na kukizunguka, kulikuwa na viumbe hai wanne. Viumbe hao walikuwa wamejaa macho mbele na nyuma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Pia mbele ya kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama bilauri. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wamejaa macho mbele na nyuma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Pia mbele ya kiti cha enzi palikuwa na kile kilichoonekana kama bahari ya kioo, iliyokuwa angavu kama bilauri. Katikati, kukizunguka kile kiti cha enzi, kulikuwa na viumbe wanne wenye uhai, wakiwa wamejawa na macho mbele na nyuma.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 4:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi.


Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.


Na mmoja wa wale nyama wane wenye uliayi akawapa vichupa saba vya dhahabu, vimejaa ghadhabu ya Mungu aliye hayi hatta milele na milele.


Na wale wazee ishirini na wane, na wale nyama wane wenye uhayi wakasujudu na kumwabudu Mungu aketiye katika kiti cha enzi, wakisema, Amin, Halleluya.


wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi safi, kama bilauri:


Na majenzi ya nle ukuta ya yaspi, na mji ule dhahabu safi, mfano wa kioo safi.


Na milango thenashara, lulu thenashara: killa mlango ni lulu moja. Na njia ya mji dhahabu safi kama kioo kisichoizuia nuru.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Nikaona, nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale nyama wenye uhayi, na za wale wazee, na hesabu yao, elfu kumi marra elfu kumi, na elfu marra elfu,


Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Hatta alipokitwaa kile kitabu, nyama wane wenye uhayi na wale wazee ishirini na wane wakaanguka mbele ya Mwana Kondoo, killa mmoja wao ana kinubi, na vitupa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambavyo ni maombi ya watakatifu.


NIKAONA hapo Mwana Kondoo alipofungua moja ya zile muhuri, nikasikia mmoja wa wale nyama wenye uhayi akisema, kama sauti ya ngurumo, Njoo! uone.


Nikasikia sauti kati kati ya nyama wane wenye uhayi, ikisema, Kibaba cha nganu kwa nussu rupia, na vibaba vitatu vya shairi kwa nussu rupia, wala usiyadhuru mafuta na mvinyo.


Na malaika wote wamesimama pande zote za kiti cha enzi na za wazee na za vile viumbe vine vyenye uhayi, wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu,


Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo