Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 4:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Umeme, sauti na ngurumo, vilikuwa vinatoka kwenye hicho kiti cha enzi. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya hicho kiti cha enzi. Taa hizo ni roho saba za Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya kiti cha enzi, taa saba zilikuwa zinawaka. Hizi ndizo roho saba za Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwenye kile kiti cha enzi palikuwa panatoka miali ya umeme wa radi, ngurumo na sauti za radi. Mbele ya kiti cha enzi, taa saba zilikuwa zinawaka. Hizi ndizo roho saba za Mungu.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 4:5
24 Marejeleo ya Msalaba  

NDIPO ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.


Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia killa mmoja wao.


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Akalia kwa sauti kuu, kama simba angurumavyo. Na alipolia ugurumo saba zikatoa sauti zao.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Malaika akakitwaa cheteso akakijaza moto wa madhbahu, akautupa juu ya inchi, kukawa sauti na radi na umeme na tetemeko la inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo