Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 4:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Na marra nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na juu ya kile kiti ameketi mmoja:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mara nikakumbwa na Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mara nikakumbwa na Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mara nikakumbwa na Roho. Kumbe, huko mbinguni kuna kiti cha enzi na juu yake ameketi mmoja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Ghafula nilikuwa katika Roho wa Mungu, na hapo mbele yangu palikuwa kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Ghafula nilikuwa katika Roho, na hapo mbele yangu kilikuwepo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa na mtu.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 4:2
28 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia, Imekuwaje bassi Daud katika Roho kumwita Bwana, akinena,


BASSI, katika hayo tuuayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunae kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni,


Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, illi azaapo, amle mtoto wake. Akazaa mtoto mwanamume, atakaewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hatta kwa Mungu na kwa kiti cbake cha enzi.


Akanichukua katika Roho hatta jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu va nyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya ukafiri, mwefiye vichwa saba na pembe kumi.


Na wale wazee ishirini na wane, na wale nyama wane wenye uhayi wakasujudu na kumwabudu Mungu aketiye katika kiti cha enzi, wakisema, Amin, Halleluya.


Nikaona kiti eba enzi, cheupe, kikubwa, nae aketiye juu yake; inchi na mbingu zikakimbia nso wake, na mahali pao hapakuonekana.


Akanichukua katika Roho hatta mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemi, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyiezi Mungu,


Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,


Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.


Na hawa nyama wenye uhayi watakapompa yeye aketiye juu ya kiti cha enzi yeye aliye hayi hatta milele na milele ntukufu na heshima na shukrani,


NIKAONA katika mkono wa kuume wa aliyeketi juu ya kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.


Na killa kiumbe kilicho mbinguni na juu ya inchi na chini ya inchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na una Mwana Kondoo hatta milele na milele.


wakaiambia milima na miamba, Tuangukieni, katusetirini, tusione uso wake aketiye juu ya kiti cha enzi wala hasira ya Mwana Kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo