Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 4:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu, nami nitakuonesha mambo yatakayotukia baadaye.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu, nami nitakuonesha mambo yatakayotukia baadaye.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Baada ya hayo nilitazama nikaona mlango umefunguliwa mbinguni. Na ile sauti niliyoisikia pale awali ambayo ilikuwa kama sauti ya tarumbeta, ikasema, “Njoo hapa juu, nami nitakuonesha mambo yatakayotukia baadaye.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango uliokuwa wazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo mwanzo ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo huku, nami nitakuonesha yale ambayo hayana budi kutendeka baada ya haya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Baada ya mambo hayo nilitazama, nami nikaona mbele yangu mlango uliokuwa wazi mbinguni. Nayo ile sauti niliyokuwa nimeisikia hapo mwanzo ikisema nami kama tarumbeta ikasema, “Njoo, huku, nami nitakuonyesha yale ambayo hayana budi kutokea baada ya haya.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 4:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nae Yesu alipokwisha kubatizwa marra akapanda kutoka majini: mbingu zikamfunukia, akamwona Roho ya Mungu akishuka kama hua, akija juu yake:


Marra akapanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kwa mfano wa hua, akishuka juu yake;


Na watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu nae akiisha kubatizwa, na akisali, mbingu zilifunuka.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


na chombo kikimshukia kama nguo kubwa, kinatelemshwa kwa pembe zake nne hatta inchi.


Akasema, Tazama! naona mbingu zimefunuliwa, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa Mungu.


Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, nikaona vinara saba vya dhahabu;


Bassi, yaandike mambo uliyoyaona, nayo yatakayokuwa baada ya hayo.


Nikasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hatta huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.


Hekalu ya Mungu ikafunguliwa mbinguni na sanduku la agano likaonekana ndani ya hekalu yake. Kukawa umeme, na sauti, na radi, na tetemeko, na mvua ya mawe uyingi sana.


Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.


Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.


Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo