Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: “Mimi niliye mtakatifu na wa kweli, ambaye nina ule ufunguo wa Daudi na ambaye hufungua na hakuna awezaye kufunga, hufunga na hakuna awezaye kufungua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: “Mimi niliye mtakatifu na wa kweli, ambaye nina ule ufunguo wa Daudi na ambaye hufungua na hakuna awezaye kufunga, hufunga na hakuna awezaye kufungua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: “Mimi niliye mtakatifu na wa kweli, ambaye nina ule ufunguo wa Daudi na ambaye hufungua na hakuna awezaye kufunga, hufunga na hakuna awezaye kufungua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Filadelfia, andika: Haya ndio maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Filadelfia, andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, yeye aliye na ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, wala anachokifunga hakuna awezaye kukifungua.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:7
38 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litafungwa mbinguni: na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.


Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe.


akinena, Tʼuna nini nawe, Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


Huyu atakuwa mkuu, atakwitwa Mwana wake Aliye juu; na Bwana Mungu atampa kiti cha Daud baba yake.


Ah, tuna nini nawe Yesu Mnazareti? umekuja kutuangamiza? Nakutambua wewe, Mtakatifu wa Mungu.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Ninyi mlimkana yule Mtakatifu, yule Mwenye haki, mkataka mpewe muuaji:


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako.


Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.


kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki: maana amemhukumu yule kahabu mkuu aliyeiharibu inchi kwa uasharati wake, na kumpatiliza kwa ajili va damu ya watumwa wake mkononi mwake.


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu.


Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu.


Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Wakalia kwa sauti kuu, wakiseina, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hatta lini huhukumu na kuipatia haki damu yetu kwao wakaao juu ya inchi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo