Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Lakini unayo majina machache, hatta katika Sardi, watu wasioyatia uchafu mavazi yao. Nao watakwenda pamoja nami katika mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wamevaa mavazi meupe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wamevaa mavazi meupe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Lakini wako wachache huko Sarde ambao hawakuyachafua mavazi yao. Hao wanastahili kutembea pamoja nami wamevaa mavazi meupe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 “Lakini bado una watu wachache katika Sardi ambao hawajayachafua mavazi yao. Wao wataenda pamoja nami, wakiwa wamevaa mavazi meupe, kwa maana wanastahili.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:4
31 Marejeleo ya Msalaba  

Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu amini; kakaeni humo hatta mtakapotoka.


Na wakiingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe: wakastaajabu.


bali wao watakaohesabiwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaozwi,


Kwa hiyo kesheni killa wakati, mkiomba mpate kuhesabiwa kuwa mmestahili kuponea haya yote yatakayokuwa, na kusimama mahali penu mbele ya Mwana wa Adamu.


Siku zile akasimama Petro kati ya wanafunzi, akasema (jumla ya majina ilipata mia na ishirini),


ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa;


bali wengine waokoeni kwa khofu, mkiwanyakua katika moto, mkilichukia hatta vazi lililotiwa takataka na mwili.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo.


Na majeslii yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa katani safi, nyeupe.


Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.


Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,


Yeye ashindae atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitaliungama jina lake mbele za Baba yaugu, na mbele ya malaika zake.


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Wakapewa killa mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hatta itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao watakaouawa vile vile kama wao.


Baada ya haya nikaona, na tazama mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezae kuuhesabu, watu wa killa taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo