Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u maskini, na mtu wa kuhurumiwa, na mhitaji, na kipofu, na nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Wewe unajisema, ‘Mimi ni tajiri; ninajitosheleza, sina haja ya kitu chochote;’ kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa, maskini, kipofu tena uko uchi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Wewe unajisema, ‘Mimi ni tajiri; ninajitosheleza, sina haja ya kitu chochote;’ kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa, maskini, kipofu tena uko uchi!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Wewe unajisema, ‘Mimi ni tajiri; ninajitosheleza, sina haja ya kitu chochote;’ kumbe, hujui kwamba wewe ni mnyonge, unahitaji kuhurumiwa, maskini, kipofu tena uko uchi!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu chochote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu chochote.’ Lakini hutambui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:17
26 Marejeleo ya Msalaba  

Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Nae Yesu akisikia, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.


Wenye njaa amewashibisha mema; Wenye mali amewaondoa mikono mitupu


Bali ole wemi ninyi mlio na mali: kwa sababu mmekwisha kuwa na faraja yenu.


Marra haba. Yalikatiwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune bali uogope;


Kwa maana sitaki ndugu msiijue siri hii, ms jione kuwa wenye akili, ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka ntimilifu wa mataifa uwasili;


Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia killa mtu alioko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyoamgawi killa mtu kadiri ya imani.


Ole wangu mimi bin Adamu! nani atakaeniokoa na mwili huu wenye kunifisha.


Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.


Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake.


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


Bassi, kwa sababu una uvuguvugu, wala huwi baridi wala moto, nitakutema kama mate katika kinywa changu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo