Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Najua matendo yako, ya kuwa huwi baridi wala hu moto; ingekuwa kheri kama ungekuwa baridi au moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: Baridi au moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: Baridi au moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: baridi au moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Nayajua matendo yako, kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa moto au baridi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Nayajua matendo yako, ya kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungelikuwa moja au lingine.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:15
23 Marejeleo ya Msalaba  

Apendae baba au mama kuliko mimi, hanifai; na apendae mwana au binti kuliko mimi hanifai.


Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, pendo la watu wengi litapoa.


Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;


Mtu aliye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo, na awe anathema. Maranatha.


Maana naogopa, nisije nikawakuta si kama vile nitakavyo kuwakuta, nikaonekane kwenu si kama vile mtakavyo: nisije nikakuta labuda fitina, na wivu, na hasira, na ugomvi, na masingizio, na manongʼonezo, na majivuno, na ghasia;


Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


mtu wa nia mbili asitasita katika njia zake zote.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;


Lakini nina neno jun yako, kwa sababu umeacha npendo wako wa kwanza.


NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.


Bassi, kwa sababu una uvuguvugu, wala huwi baridi wala moto, nitakutema kama mate katika kinywa changu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo