Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andika hivi: “Mimi niitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyote alivyoumba Mungu nasema hivi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andika hivi: “Mimi niitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyote alivyoumba Mungu nasema hivi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikea andika hivi: “Mimi niitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, ambaye ni chanzo cha viumbe vyote alivyoumba Mungu nasema hivi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Laodikia, andika: Haya ndio maneno yake yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Laodikia, andika: “Haya ndiyo maneno yake yeye aliye Amen, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa uumbaji wote wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:14
22 Marejeleo ya Msalaba  

Vyote vyalifanyika kwa huyu. Wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako.


Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.


nae ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.


Nae ni kichwa cha mwili, yaani cha kanisa; nae ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, illi awe mtangulizi katika yote.


MAANA nataka muijue juhudi niliyo nayo kwa ajili yenu, na kwa ajili ya wale wa Laodikia, na wale wasioniona uso wangu katika mwili, jinsi ilivyo kuu;


Waraka hun ukiisha kusomwa kwenu, fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama farasi mweupe, nae aliyempanda, aitwae Mwaminifu na wa kweli, nae kwa haki ahukumu na kufanya vita.


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.


Mimi Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho.


Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Filadelfia andika; Haya ayanena yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daud, mwenye kufungua wala hapana afungae, nae afunga wala hapana afuuguae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo