Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:11 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

11 Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Naja kwako upesi! Shikilia kwa nguvu ulicho nacho sasa, ili usije ukanyang'anywa na mtu yeyote taji yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Naja kwako upesi! Shikilia kwa nguvu ulicho nacho sasa, ili usije ukanyang'anywa na mtu yeyote taji yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Naja kwako upesi! Shikilia kwa nguvu ulicho nacho sasa, ili usije ukanyang'anywa na mtu yeyote taji yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akalichukua taji lako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 “Ninakuja upesi. Shika sana ulicho nacho, ili mtu asije akaichukua taji yako.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:11
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na killa ashindanae hujiweza katika yote: bassi hao kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi isiyoharibika.


Upole wenu ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu.


Hatta mtu akishindana hapewi taji asiposhindana kwa halali.


baada ya haya nimewekewa taji ya baki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa katika siku ile: wala si mimi tu, bali watu wote pia waliopenda kutokea kwake.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Msinungʼunikiane, ndugu, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.


Tazama, naja kama mwizi. Yu kheri akeshae, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi wakaone aibu yake.


Usiogope mambo yatakavokupata: tazama mshitaki atawatupa baadhi yenu gerezani illi mjaribiwe, nanyi mtakuwa na mateso siku kumi. Uwe mwaminifu hatta kufa, nami nitakupa taji ya uzima.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Illa mlicho nacho kishikeni, hatta nitakapokuja.


Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa killa mtu kama itakavyokuwa kazi yake.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako.


ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo