Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 3:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 “Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 “Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 “Kwa malaika wa kanisa la Sarde andika: “Mimi niliye na roho saba za Mungu na nyota saba, nasema hivi: Nayajua mambo yako yote; najua unajulikana kuwa na uhai kumbe umekufa!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Sardi, andika: Haya ndio maneno ya aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Sardi, andika: “Haya ndiyo maneno ya aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, kwamba una sifa ya kuwa hai, lakini umekufa.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 3:1
30 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana. Wakaanza kufanya furaha.


Tena kufanya furaha na kuona furaha kulikuwa wajib, kwa maana huyu ndugu yako alikuwa amekufa, nae amefufuka: alikuwa amepotea, nae ameonekana.


Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu.


Akiisha kusema haya, akawapulizia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


NA ninyi, mlipokmva wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zemi,


hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);


Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hayi pamoja nae, akiisba kuwasameheni makosa yote;


Na yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hayi.


Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


Watu hawa ni miamba yenye khatari katika karamu zenu za upendo wafanyapo karamu pamoja nanyi, wakijilisha pasipo khofu; ni mawingu yasiyo na maji, yachukuliwayo na upepo; ni miti iliyopukutika, isiyo na matunda, iliyokufa marra mbili, na kungʼolewa kabisa;


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.


Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Najua matendo yako na upendo wako na khuduma yako na uaminifu wako na uvumilivu wako na matendo yako; tena matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.


Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


Najua matendo yako, ya kuwa huwi baridi wala hu moto; ingekuwa kheri kama ungekuwa baridi au moto.


Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe manibo yaliyosalia, yaliyo tayari kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu.


Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.


Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na ngurumo na sauti. Na taa saha za moto zikiwaka mbele ya kiti kile cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo