Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 22:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Akaniambia, Haya ni maneno ya uaminifu na ya kweli. Na Bwana Mungu wa manabii watakatifu alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake mambo ambayo hayana buddi kuwa upesi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Kisha malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kweli na ya kuaminika. Bwana Mungu ambaye huwapa manabii Roho wake, alimtuma malaika wake awaoneshe watumishi wake mambo ambayo lazima yatukie punde.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Mwenyezi Mungu, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kisha yule malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. bwana Mwenyezi, aliye Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumishi wake yale ambayo hayana budi kutukia upesi.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:6
26 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya katika ufalme wake machukizo yote, nao watendao maasi,


(Kama alivyosema kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu mwanzo),


Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.


Hatta Petro alipofahamu akasema, Sasa nimejua yakini ya kuwa Bwana amempeleka malaika wake na kunitoa katika mkono wa Herode na kutazamia kwa taifa la Wayahudi.


Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.


ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,


Na roho za manabii huwatii manabii.


Lakini, nasema hivi, ndugu, muda ubakio si mwingi; bassi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana;


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


Na pamoja na haya tulikuwa na baba za mwili wetu walioturudi, tukawastahi; bassi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi.


Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


mpate kuyakumbuka maneno yaliyonenwa zamani na manabii watakatifu, na ile amri ya Bwana Mwokozi iliyoletwa na mitume wake.


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.


Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.


Na yeye aketiye juu ya kiti cha enzi akasema, Tazama, nafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika, kwa maana haya ni maneno ya kweli, na ya uaminifu.


Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


BAADA ya haya naliona, na tazama mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hatta huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana buddi kuwa baada ya bayo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo