Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 22:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, maana Bwana Mungu atawaangazia, nao watatawala milele na milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yao, nao watatawala milele na milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu atakuwa nuru yao, nao watatawala milele na milele.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:5
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


wala nuru ya taa haitamulika ndani yako tena kabisa, wala sauti ya bwana arusi na bibi arusi haitasikiwa ndani yako tena kabisa; maana wafanyi biashara wako walikuwa wakuu wa inchi, kwa kuwa mataifa yote wamedanganywa kwa uchawi wako.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.


wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi safi, kama bilauri:


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo