Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 22:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Na watumishi wake watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake katika vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Watauona uso wake, na jina lake litaandikwa juu ya paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 nao watamwona uso wake na Jina lake litakuwa kwenye paji za nyuso zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 nao watamwona uso wake na Jina lake litakuwa kwenye vipaji vya nyuso zao.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wa kheri walio na moyo safi; maana hawo watamwona Mungu.


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule uso kwa uso: wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana jinsi ninavyojuliwa na mimi sana.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


NIKAONA, na tazama, Mwana kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arubaini na nne elfu pamoja nae, wenye jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.


Yeye ashindae, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, Yerusalemi ulio mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.


akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo