Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 22:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa killa mtu kama itakavyokuwa kazi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:12
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.


Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.


Bassi yeye apandae, na yeye atiae maji ni kitu kimoja, na killa mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.


Na mataifa walighadhabika, ghadhabu yako ikaja, na wakati wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, nao walichao jina lako, wadogo na wakubwa, na wa kuwaharibu hawo waiharibuo inchi.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo