Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 22:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Akaniambia, Msiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Tena akaniambia, “Usiyafiche kama siri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, maana wakati wa kutimizwa kwake umekaribia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kisha akaniambia, “Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu wakati umekaribia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kisha akaniambia, “Usiyafunge maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, kwa sababu wakati umekaribia.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:10
21 Marejeleo ya Msalaba  

Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni kalika nuru; na msikialo kwa siri, likhubirini juu ya nyumba.


Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini.


Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.


Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.


Hatta ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika.


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Namshuhudia killa mtu ayasikiae maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu aliye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Akaniambia, Angalia, usifanye hivyo; mimi mjoli wako, na wa ndugu zako manabii na wa wale washikao maneno ya kitabu hiki. Msujuduni Mungu.


NIKAONA katika mkono wa kuume wa aliyeketi juu ya kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo