Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 21:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Kisha akaniambia, “Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uhai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yoyote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Akaniambia, “Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Yeye aonaye kiu nitampa kunywa kutoka chemchemi ya maji ya uzima bila gharama yoyote.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 21:6
26 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi?


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


wanapewa haki burre kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Yesu Kristo:


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.


Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huu dhahabu au fedha au vitu vya thamani au miti au majani an manyasi,


Bassi, asijisifu mtu katika wana Adamu.


Bassi Apollo ni nani? na Paolo ni nani? Ni wakhudumu ambao kwao mliamini; na killa mtu kama Bwana alivyompa.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Na nilipomwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akiniambia, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


akaapa kwa yeye aliye bayi hatta milele na milele, aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na inchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na muhulla baada ya haya,


Malaika wa saba akakimimina kichupa chake katika hewa. Sauti kuu ikatoka katika hekalu ya mbinguni, kalika kiti kile cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.


Mimi Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, wa kwanza na wa mwisho.


Na Roho na Bibi arusi wasema, Njoo. Nae asikiae aseme, Njoo. Nae aliye na kiu, na aje: na apendae ayatwae maji ya uzima burre.


Na kwa Kanisa lililo katika Laodikia andika; Haya ayanena yeye aliye Amin, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa viumbe vya Mungu.


Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo