Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 21:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 21:4
26 Marejeleo ya Msalaba  

Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe.


Adui wa mwisho atakaebatilishwa ni mauti.


Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.


Hatta imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya, vya kale vimepita; kumbe! vyote vimekuwa vipya.


Kwa hiyo Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, Wala msiguse kitu kilicho kichafu.


Neno lile, Marra moja tena, ladhihirisha kuhamishwa vile viwezavyo kutetemeshwa, kama vitu vilivyoumbwa, illi vitu visivyoweza kutetemeshwa vikae.


Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.


Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele.


Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.


Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.


NIKAONA mbingu mpya na inchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na inchi za kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.


Wala hapatakuwa laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana kondoo kitakuwa ndani yake.


Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo