Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 21:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wana Adamu, nae atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, Mungu wao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, “Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 21:3
29 Marejeleo ya Msalaba  

Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.

Yesu akajibu akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.

Kwa maana ninyi hekalu la Mungu aliye hayi; kama Mungu alivyosema, ya kama, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

Nami nitawakaribisheni, Nitakuwa Baba kwenu, Na ninyi mtakuwa kwangu wana na binti, anena Bwana Mwenyiezi.

Bassi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu Kristo atuongoze njia yetu tufike kwenu;

Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.

Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.

mkhudumu wa patakatifu, na wa khema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwana Adamu.

Hatta ngurumo saba zilipotoa sauti zao, nalikuwa tayari kuandika.

Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, kitwae kile kitabu kidogo kilichofunuliwa katika mkono wa yule malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya inchi.

Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikinena, Sasa kumekuwa wokofu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake: kwa maana ametupwa mshitaki wa ndugu zetu, awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchaua na nsiku.

Yeye ashindae atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, nae atakuwa Mwana wangu.

Wala hapatakuwa laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana kondoo kitakuwa ndani yake.

Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda khema yake juu yao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo