Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 21:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyae machukizo na uwongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Lakini hakuna chochote kilicho najisi kitakachoingia humo; wala mtu yeyote atendaye mambo ya kuchukiza au ya uongo hataingia humo. Ni wale tu walioandikwa katika kitabu cha uhai cha Mwanakondoo ndio watakaoingia ndani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu yeyote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Lakini kitu kichafu hakitaingia humo kamwe, wala mtu yeyote atendaye mambo ya aibu au ya udanganyifu. Bali watakaoingia humo ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 21:27
28 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watakusanya katika ufalme wake machukizo yote, nao watendao maasi,

wakaona baadhi ya wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najis, yaani, yasiyonawiwa, wakawalaumu.

Lakini msifurahi kwa sababu hii ya kuwa pepo wanawatiini: hali furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.

Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.

Naam, nakutaka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi nae, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.

na wazinzi, na wafiraji, na waibao watu, na wawongo, mi waapao uwongo, na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima;

Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;

Lakini, kwa sababu ya ahadi yake tunatazamia mbingu mpya na inchi mpya, ambayo haki itakaa ndani yake.

Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.

Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.

Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.

Yeye ashindae atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitaliungama jina lake mbele za Baba yaugu, na mbele ya malaika zake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo