Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 21:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Mji huo hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, maana utukufu wa Mungu huuangazia, na taa yake ni yule Mwanakondoo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Ule mji hauhitaji jua wala mwezi kuuangazia, kwa sababu utukufu wa Mungu ndio nuru yake na Mwana-Kondoo ndiye taa yake.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 21:23
25 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.


Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu,


Kulikuwako nuru halisi, imtiayo nuru killa mtu ajae katika ulimwengu.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Na nilipokuwa sioni kwa sababu ya fakhari ya nuru ile, nikaongozwa na mikono yao waliokuwa pamoja nami, nikafika Dameski.


Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo.


BAADA ya haya nalioua malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu, inchi ikaangazwa kwa utukufu wake.


wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi safi, kama bilauri:


Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo