Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 21:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyiezi ni hekalu lake, na Mwana kondoo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Sikuona hekalu katika mji huo, maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu na yule Mwanakondoo ndio hekalu lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Sikuona hekalu katika mji huo, maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu na yule Mwanakondoo ndio hekalu lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Sikuona hekalu katika mji huo, maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu na yule Mwanakondoo ndio hekalu lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio Hekalu lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu bwana Mwenyezi Mungu na Mwana-Kondoo ndio hekalu lake.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 21:22
25 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitahomolewa.


Mimi na Baba yangu tu nmoja.


Mungu akiwa ametukuzwa ndani yake, Mungu nae atamtukuza ndani ya nafsi yake; na marra atamtukuza.


Yesu akamwambia, Ee mwanamke, uniamini, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala katika Yerusalemi.


Lakini saa inakuja, na sasa ipo, ambayo wenye ibada khalisi watamwabudu Baba katika roho na kweli: kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.


Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae,


Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa namna ya kimwili.


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


wakisema, Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyiezi, ulioko, na nliyekuwako, kwa sababu umetwaa uweza wako ulio mkuu, ukamiliki.


Hawa udio wasiotiwa najis pamoja na wanawake, kwa maana ni bikira. Hawa ndio wamfuatao Mwana kondoo killa aendako. Hawa walinunuliwa katika inchi, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana kondoo.


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Maana udizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa inchi na wa ulimwengu wofe, kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyiezi.


Nikaisikia madhbahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyiezi, za kweli, za haki hukumu zako.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.


Nikaona, na tazama, kati kati ya kiti cha enzi na ya nyama wane wenye uhayi, na kati kati ya wale wazee, Mwana Kondoo, amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.


Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda khema yake juu yao.


Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo