Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 21:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwa Mungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi arusi aliyepambwa tayari kukutana na mumewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nikauona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Nikaona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 21:2
28 Marejeleo ya Msalaba  

Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; maana naliwaposea mume mmoja, nimletee Kristo bikira safi.


Maana waliutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuujenga na kuufanyiza ni Mungu.


Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.


Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye tiayi, Yerusalemi wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,


Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao.


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Yohana kwa makanisa saba yaliyo katika Asia: Neema iwe kwenu na amani zitokazo kwake yeye alioko na aliyekuwako nii atakaekuwako: na zitokazo kwa roho saba zilizo mbele ya kiti chake cha enzi:


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Na behewa iliyo nje ya hekalu uitupe nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.


Akanichukua katika Roho hatta mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemi, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyiezi Mungu,


Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.


Na Roho na Bibi arusi wasema, Njoo. Nae asikiae aseme, Njoo. Nae aliye na kiu, na aje: na apendae ayatwae maji ya uzima burre.


Na mtu aliye yote akiondoa baadhi ya maaeno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika kile kitabu cha uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao khabari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.


Yeye ashindae, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, Yerusalemi ulio mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo