Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 21:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 ulikuwa ua ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango thenashara, na katika ile milango malaika thenashara, na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila thenashara za wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Ulikuwa na ukuta mrefu na mkubwa, wenye milango kumi na miwili, na kila mmoja ulilindwa na malaika. Juu ya kila mlango paliandikwa mojawapo ya majina ya makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye malango kumi na mawili, pakiwa na malaika kumi na wawili kwenye hayo malango. Kwenye malango hayo yaliandikwa majina ya yale makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 21:12
21 Marejeleo ya Msalaba  

Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.

Ikawa maskini akafa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa Ibrahimu. Akafa na yule tajiri, akazikwa.

ambayo kabila zetu thenashara wanataraja kuifikia, wakimkhudumu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, ee Mfalme.

Hawo wote si roho zitumikazo, wakitumwa kuwakhudumu wale watakaourithi wokofu?

Upande wa mashariki milango mitatu: na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu: na upande wa magharibi milango mitatu.

Na yeye aliyenena nami alikuwa na mwanzi wa dhababu apate kuupima mji na milango yake na ukuta wake.

Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.

Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo