Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 20:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Wameneemeka sana, tena heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wa kwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Al-Masihi, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka elfu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Al-Masihi, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 20:6
19 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi mtu mmoja katika hawo walioketi pamoja nae, alipoyasikia haya, akamwambia, Yu kheri atakaekula mkate katika ufalme wa Mungu.


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hayi, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani utakatifu, mtoe dhabibu za roho, zipatazo kibali kwa Mungu, kwa Yesu Kristo.


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa killa kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo