Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 20:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu hao walipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwa wamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamu yake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji za nyuso zao, au juu ya mikono yao. Walipata tena uhai, wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka 1,000.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kisha nikaona viti vya utawala vilivyokuwa vimekaliwa na wale waliopewa mamlaka ya kuhukumu. Tena nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Isa na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudu huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye paji za nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Al-Masihi miaka elfu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu, na nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Isa na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudu huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Al-Masihi miaka 1,000.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 20:4
40 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Ndipo wengi watajikwaa, na watasalitiana, na kuchukiana.


Lakini Herode aliposikia, alinena, Huyu ndiye Yohana, niliyemkata kichwa; amefufuka.


Marra mfalme akatuma askari, akiamuru kuleta kichwa chake.


Wakamhoji, wakinena, Waandishi wanena ya kuwa imempasa Eliya kuja kwanza.


Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa.


kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.


mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na kuketi katika viti vya enzi, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi.


Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhayi baada ya kufa?


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


aliyeshuhudia Neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo, mambo yote aliyoyaona.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Na baada ya siku tatu u nussu roho ya uhayi itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama, khofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


Nami nitawarukhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na miateen na sittini, wamevikwa mavazi ya kigunia.


Hatta watakapoumaliza ushuhuda wao yule nyama atokae katika abuso atafanya vifa nao, nae atawashinda na kuwaua.


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Na moshi wa maumivu yao wapanda juu hatta milele na milele, nao bawana raha mchana na usiku, bao wamsujuduo nyama na sanamu yake, na killa aipokeae alama ya jina lake.


Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Na yeye ashindae na kuyatunza matendo yangu hatta mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,


Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Na viti ishirini na vine vilikizuniguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wane, wamekeli, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu.


Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhbahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


akisema, Msiidhuru inchi wala bahari wala miti hatta tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mwenyiezi Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo