Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 20:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kisha Kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kisha Kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kisha Kifo na Kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili la moto ndicho kifo cha pili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 20:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Adui wa mwisho atakaebatilishwa ni mauti.


Maana sharti huu wenye uharibifu uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.


Yule nyama akakamatwa, na nabii wa uwongo aliye pamoja nae, yeye aliyezifanya ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile alama ya nyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa hayi katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.


Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.


Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.


Nae atafuta killa chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena: wala maombolezo, wala kilio, wala taabu haitakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo