Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka, ukatubu na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kumbuka basi ni wapi ulikoanguka! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kumbuka basi ni wapi ulikoangukia! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:5
34 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kustirika ukiwa juu ya mlima.


Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani.


Bassi atafanyani yule Bwana wa mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa watu wengine.


Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa.


Atakuja na kuwaangamiza wale wakulima, na lile shamba la mizabibu atawapa wengine.


Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.


mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala ndanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, na kilichopotoka; kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima;


Lakini zikumbukeni siku za kwanza, ambazo, mlipokwisha kutiwa nuru, mlistahimili mashindano makubwa ya maumivu;


Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhababu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na vile vinara saba ulivyoviona ni makanisa saba.


Wana Adamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo yote, wala hawtikutubu na kumpa utukufu.


Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.


Najua matendo yako na upendo wako na khuduma yako na uaminifu wako na uvumilivu wako na matendo yako; tena matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.


Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;


Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo