Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 2:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 “Lakini nyinyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezebeli na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 “Lakini nyinyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezebeli na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 “Lakini nyinyi wengine mlioko huko Thuatira ambao hamfuati mafundisho yake Yezebeli na ambao hamkujifunza kile wanachokiita Siri ya Shetani, nawaambieni kwamba sitawapeni mzigo mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo yanayoitwa mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wowote juu yenu):

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo yanayoitwa mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wowote juu yenu):

Tazama sura Nakili

Ufunuo 2:24
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo illa hayo yaliyo faradhi,

Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo.

Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho yake. Maana Roho huchunguza yote, hatta mafumbo ya Mungu.

Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.

Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana sisi si wajinga, tunajua fikara zake.

Hekima hii siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, na ya tabia ya kibinadamu, na ya Shetani,

ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.

Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.

Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Thuatera andika, Haya ayanena Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho kama mwako wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.

Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo