Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Nami nitawaua watoto wake. Nayo makundi yote ya waumini yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Nami nitawaua watoto wake. Nayo makundi yote ya waumini yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:23
39 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Akawaambia, Ninyi ndio watu wanaodai kuwa wenye haki mbele ya wana Adamu, lakini Mungu anajua mioyo yenu; kwa maana lililotukuka kwa wana Adamu, ni chukizo mbele ya Mungu.


Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.


Yesu akamwambia, Enenda, kamwite mume wako uje nae hapa.


Wakasali, wakasema, Wewe, Bwana, ujuae mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,


Bassi kama ni hivyo, killa mtu miongoni mwetu atatoa khabari za nafsi yake mbele za Mungu.


Na yeye aichunguzae mioyo aijua nia ya Roho, ya kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


Maana killa mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.


Wala hakuna kiumbe kisicho wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu, na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.


Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni;


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Yeye alive na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae, nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio kati kati va bustani ya Mungu.


Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.


Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.


Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami kumlipa killa mtu kama itakavyokuwa kazi yake.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo