Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Najua mambo yako yote; najua bidii yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni waongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba umewajaribu wale wanaojifanya mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:2
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwafahamu ninyi wakati wo wote: ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.


Alinena haya illi amjaribu: kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda.


mkageukia injili ya namna nyingine; wala si nyingine. Lakini wapo watu wawataabishao na watakao kuigeuza injili ya Kristo.


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


jaribuni vyote; lishikeni lililo jema;


Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


Lakmi unalo neno hili kwamba wayachukia matendo ya Wanikolaiti, niyachukiayo na mimi.


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


NA kwa malaika wa kanisa lililo katika Sardi, andika; Haya ayanena yeye aliye nazo roho saba za Mungu na zile nyota saba: Najua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hayi, nawe umekufa.


Najua matendo yako, ya kuwa huwi baridi wala hu moto; ingekuwa kheri kama ungekuwa baridi au moto.


Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo