Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Thuatera andika, Haya ayanena Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho kama mwako wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosuguliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosuguliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Kwa malaika wa kanisa la Thuatira andika hivi: “Huu ndio ujumbe wa Mwana wa Mungu, ambaye macho yake yametameta kama moto, na miguu yake inang'aa kama shaba iliyosuguliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Thiatira, andika: Haya ndio maneno ya Mwana wa Mungu, ambaye macho yake ni kama mwali wa moto, na ambaye miguu yake ni kama shaba iliyosuguliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “Kwa malaika wa kundi la waumini lililoko Thiatira, andika: “Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, ambaye macho yake ni kama mwali wa moto, na ambaye miguu yake ni kama shaba iliyosuguliwa sana.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:18
22 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.


Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabbi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israeli.


je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu.


Amin, amin, nawaambieni, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hayi.


Mwanamke mnioja, jina lake Ludia, mwenye kuuza rangi ya zambarao, mwenyeji wa Thuatira, mcha Mungu, akatusikiliza. Moyo wake huyu ukafunguliwa na Bwana, ayaangalie mineno yaliyonenwa na Paolo.


Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


KWA malaika wa kanisa lililo katika Efeso andika; Haya ayanena yeye azishikae nyota saba katika mkono wake wa kuume, aendae kati kati ya vile vinara saba vya dhahabu.


Lakini nawaambia ninyi, nao wengine walio katika Thuatera, wo wote wasio na mafundisho haya, wasiozijua fumbo za Shetani kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yen umzigo mwungine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo