Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 “Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi nitampa ile mana iliyofichika. Nitampa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 “Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi nitampa ile mana iliyofichika. Nitampa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 “Aliye na masikio, basi, na asikie yale Roho anayoyaambia makanisa! “Mshindi nitampa ile mana iliyofichika. Nitampa pia jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya ambalo hakuna mtu aliyelijua isipokuwa tu wale wanaolipokea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho wa Mungu ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 “Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makundi ya waumini. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 2:17
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.

Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie.

Akawaambia, Mimi nina chakula msichokijua ninyi.

Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

nao waimba wimbo niliouona kuwa mpya mbele ya kili cha enzi, na mbele ya wale nyama wane wenye uhayi, na wale wazee; na hapana mtu aliyeweza kujifunza uimbo ule illa wale mia na arubaini na nne elfu walionunuliwa katika inchi.

Nae ana jina limeandikwa katika vazi lake mi paja vake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.

Yeye alive na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae, nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio kati kati va bustani ya Mungu.

Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo