Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Basi, tubu. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Basi, tubu. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Basi, tubu. La sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Basi tubu! Ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Basi tubu! Ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Tena ipokeeni chepeo ya wokofu, na upanga wa Roho, ndio neno la Mungu;


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;


Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.


Wana Adamu wakaunguzwa maunguzo makubwa, wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo yote, wala hawtikutubu na kumpa utukufu.


Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.


na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya farasi yule, utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Pergamo, andika; Haya ayanena yeye aliye na upanga mkali, mkali kuwili;


Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Mimi nawakemea wote niwapendao, na kuwarudi: bassi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo