Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaam, yeye aliyemfundisha Balak atie ukwazo mbele ya wana wa Israeli, wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Lakini ninayo machache dhidi yako: Baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu na kufanya uzinzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Lakini ninayo machache dhidi yako: Baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu na kufanya uzinzi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Lakini ninayo machache dhidi yako: baadhi yenu ni wafuasi wa Balaamu aliyemfundisha Balaki kuwatega wana wa Israeli wale vyakula vilivyotambikiwa sanamu na kufanya uzinzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Hata hivyo, nina mambo machache dhidi yako: Unao watu wafuatao mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu na kufanya uasherati.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 “Hata hivyo, nina mambo machache dhidi yako: Unao watu wafuatao mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa kafara kwa sanamu na kufanya uasherati.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:14
30 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana buddi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletae jambo la kukosesha!


mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.


Kwa khabari za watu wa mataifa walioamini, tumekwisha kutoa hukumu yetu, wsio wasishike neno linginelo illa kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongwa, na uasharati.


Na Daud asema, Meza yao iwe tanzi na mtego, Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;


Bassi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali mtoe hukumu hii, ndugu asitiwe kitu cha kumkwaza au cha kumwangusha.


Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno ambalo ndugu yako hukwazwa au kuangushwa au kuwa dhaifu.


Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwaazalo,


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


Lakini kwa sababu ya mambo ya zina killa mtu na awe na mke wake mwenyewe, na killa mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.


Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.


tena, Jiwe lakujikwaza mguu, na mwamba wa kujiangusha; maana hujikwaza kwa neno lile, wakiliasi, nao waliwekwa wapate hayo.


walioiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaam, mwana wa Bosor, aliyependa ujira wa ndhalimu:


Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


Lakini nina maneno machache juu yako, ya kwamba wamwacha yule mwanamke Yezebel, yeye ajiitae nabii, nae awafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, illi wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Lakini nina neno jun yako, kwa sababu umeacha npendo wako wa kwanza.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo