Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa, shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa, shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Najua unakoishi: Wewe unaishi kwenye makao makuu ya Shetani! Lakini bado unashikilia jina langu; hukuikana imani yako kwangu hata siku zile Antipa, shahidi wangu mwaminifu, alipouawa pale mahali anapoishi Shetani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Ninajua unakoishi: kule Shetani ana kiti chake cha utawala. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu, hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu mkuu, anakoishi Shetani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji mkuu wenu, ambako ndiko anakoishi Shetani.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 2:13
27 Marejeleo ya Msalaba  

Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu.


Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.


Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.


Mtachukizwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.


Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi nami nilikuwa nikisimama karibu, nikikubali auawe, nikizitunza nguo zao waliomwua.


hatta hapa ana mamlaka kwa makuhani wakuu awafunge wote wakuitiao Jina lako.


jaribuni vyote; lishikeni lililo jema;


Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.


Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu.


kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba yake; ambae nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na kujisifu kwetu, kwa kutumaini mpaka mwisho.


Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?


na zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi alive mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Kwake yeye aliyetupeuda na kutuosha dhambi zetu kwa damu yake,


Nami nitawarukhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na miateen na sittini, wamevikwa mavazi ya kigunia.


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Na yule nyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubba, na kinywa chake kama kinywa cha simba; yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.


Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.


Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;


Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.


Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo