Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ufunuo 19:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Na tufurahi tukashangilie tukampe ulukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa harusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa harusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa harusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia na bibi arusi wake amejiweka tayari.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Tufurahi, tushangilie na kumpa utukufu! Kwa maana arusi ya Mwana-Kondoo imewadia na bibi arusi wake amejiweka tayari.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 19:7
29 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwana wake arusi.


na ninyi kama watu wanaomngojea bwana wao, atakapoondoka arusini, illi akija na kubisha, wamfungulie marra moja.


Aliye nae bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi anaesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi: bassi hii furaha yangu imetimia.


Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; maana naliwaposea mume mmoja, nimletee Kristo bikira safi.


Maana mume ni kichwa cha mke, kama nae Kristo ni kichwa cha kanisa; nae ni mwokozi wa mwili.


Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Muugu kwa Roho, na kujisifu katika Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili. Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili.


Na katika saa ile palikuwa na tetemeko la inchi, nalo kubwa, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka, wana Adamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliosalia wakaingiwa na khofu wakamtukuza Mungu wa mbingu.


Akaniambia, Andika, Wa kheri walioitwa kwa karamu ya arusi ya Mwana Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.


Nami Yohana nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemi mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Akaja mmoja wa wale malaika saba walio na vichupa vile saba vijaavyo yale mapigo saba ya mwisho, akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi arusi, mke wa Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo