Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Ufunuo 19:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake awapige mataifa kwa huo. Nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, nae anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ukali wa ghadhabu ya Mungu Mwenyiezi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda watu wa mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda watu wa mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Nguvu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Upanga mkali hutoka kinywani mwake, na kwa upanga huo atawashinda watu wa mataifa. Yeye ndiye atakayetawala kwa fimbo ya chuma na kuikamua divai katika chombo cha kukamulia zabibu za ghadhabu kuu ya Mungu Mwenye Nguvu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Hulikanyaga shinikizo la ghadhabu ya Mungu Mwenyezi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. “Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma.” Hulikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Ufunuo 19:15
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;

Nae alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume: na upanga mkali, mkali kuwili, watoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua likingʼaa kwa nguvu zake.

Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, illi azaapo, amle mtoto wake. Akazaa mtoto mwanamume, atakaewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hatta kwa Mungu na kwa kiti cbake cha enzi.

yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.

na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya farasi yule, utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.

Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Pergamo, andika; Haya ayanena yeye aliye na upanga mkali, mkali kuwili;

Tubu; na usipotubu naja kwako upesi, nitafanya vita juu yako kwa upanga wa kinywa changu.

nae atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyangi visetwavyo, kama mimi nilivyopokea kwa Baba yangu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo